Legend #Madonna amemhimiza #PapaLeo wa XIV kutembelea Gaza na kuleta mwanga wake kwa watoto kabla haijachelewa.
Mwimbaji huyo alitoa ombi lake kwenye Instagram, akisema Papa ndiye pekee kati yetu ambaye hawezi kunyimwa kuingia. Mwezi Julai, Papa mpya alirudia wito wake wa kusitisha mapigano Gaza baada ya watu watatu waliokuwa wakijificha katika Kanisa Katoliki jijini Gaza kuuawa katika shambulio la anga la Israel.
Kauli ya Madonna imetolewa huku Uingereza, Umoja wa Ulaya, Australia, Kanada na Japani zikitoa tamko likisema kuwa njaa inaendelea kutokea mbele ya macho yetu Gaza na kuhimiza kuchukuliwa hatua kukomesha njaa.
Israel imeendelea kukanusha kuwepo kwa njaa Gaza na imezishutumu taasisi za Umoja wa Mataifa kwa kushindwa kuchukua misaada mipakani na kuifikisha.
Kwa upande wake, Umoja wa Mataifa umesema kiwango cha misaada kinachoingia Gaza kimeendelea kuwa chini sana ya mahitaji ya lazima.