Donald Trump na Tatizo la Mshipa

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

21 hours ago
rickmedia: donald-trump-tatizo-mshipa-802-rickmedia

Ikulu ya Marekani imesema kuwa Rais Donald Trump anaugua ugonjwa sugu wa mshipa hii ikiwa ni baada ya siku kadhaa za uvumi kuhusu picha zinazoonyesha michubuko kwenye mkono wa rais huyo wa Marekani.

Inaelezwa kuwa baada ya hivi karibuni kupata uvimbe kwenye miguu yake, Trump alifanyiwa uchunguzi wa kina ikiwa ni pamoja na upimaji wa mishipa ya damu, kulingana na Katibu anayehusika na Vyombo vya Habari wa Ikulu ya White House Karoline Leavitt.

Leavitt alisema hali ya mkono wa Trump ulioonekana kuvimba ilitokana na uharibifu wa tishu kutokana na kusalimiana kwa mara kwa mara wakati akitumia dawa ya aspirini, ambayo alisema ni sehemu ya utaratibu wa kawaida wa kudhibiti moyo na mishipa.