Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Lindi imemhukumu Alli Ibrahimu Malinda (30) kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 10.
Tukio hilo lilitokea Januari 6, 2025 katika Kijiji cha Ng’apa. Hukumu imetolewa Julai 23, 2025 na Hakimu Mkazi Delphina Kimathi, baada ya upande wa Jamhuri kuthibitisha kosa hilo pasipo shaka.
Mahakama imesema kuwa adhabu hiyo ni fundisho kwa wengine na inalenga kulinda haki za watoto.