Mfungwa Aliembaka Mfungwa Mwenzie Aongezewa Adhabu ya Kifungo

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

13 hours ago
rickmedia: mfungwa-aliembaka-mfungwa-mwenzie-aongezewa-adhabu-kifungo-880-rickmedia

Mfungwa #EmmanuelMagede, ambaye tayari alikuwa anatumikia kifungo cha miaka 10 kwa kosa la kubaka mtoto, ameongezewa kifungo kingine cha miaka 12 baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mfungwa mwenzake katika gereza la Harare Remand Prison.

Mahakama imeamuru pia adhabu yake ya zamani ambayo ilikuwa imesitishwa irejeshwe, hivyo sasa atalazimika kutumikia jumla ya miaka 22 jela.

Mashahidi ambao ni wafungwa wenzake walieleza kumwona akimlawiti mfungwa mwenzake bafuni wakati akifanya usafi wa mwili. Mahakama ilisisitiza kuwa kitendo hicho kilikuwa cha kinyama na kisichokubalika, hususan kwa mtu ambaye tayari alikuwa amehukumiwa kwa kosa la ubakaji muda mfupi kabla.