Diamond Afunguka kutokumshirikisha Mama Yake wakati wa Ndoa na Zuchu

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

16 hours ago
rickmedia: diamond-afunguka-kutokumshirikisha-mama-yake-wakati-ndoa-zuchu-864-rickmedia

Msanii maarufu wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul Juma maarufu kama Diamond Platnumz, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu ndoa yake na mwanamuziki mwenzake Zuchu. Diamond amesema kuwa aliamua kuoa bila hata kumjulisha mama yake mpaka pale ndoa hiyo ilipokamilika.

Akizungumza kwenye kipindi cha #WayUpWithYEE, Diamond alieleza kuwa uamuzi huo ulitokana na msukumo wa moyo na hali ya mapenzi waliyonayo, na kwamba hakutaka ucheleweshaji au ushawishi wowote kutoka kwa mtu yeyote, hata mama yake mzazi, ambaye amekuwa na nafasi kubwa katika maisha yake.

"Nilijikuta tu nimeamua. Sikumwambia mama hadi kila kitu kilipokamilika. Baada ya ndoa ndipo nilimpigia simu nikamwambia nimeshaoa," alisema Diamond.

Taarifa hiyo imeibua hisia tofauti kutoka kwa mashabiki mitandaoni, huku wengi wakimpongeza kwa kuchukua hatua ya kuanzisha familia rasmi, huku wengine wakielezea mshangao wao kutokana na ukimya ulioambatana na tukio hilo kubwa.