Mpenzi wa zamani wa #Diddy, #GinaHuynh aliyesajiliwa kama Mhusika Namba 3 katika mashitaka ya shirikisho upande wa #Diddy wakati anapojaribu kupata dhamana ili asubiri hukumu akiwa nje ya gereza.
Katika nyaraka mpya za kisheria zilizopatikana na TMZ, Gina ameandika barua kwa jaji akiunga mkono ombi la Diddy la kupewa dhamana.
Anasema amemfahamu Diddy kwa miaka mingi na anamchukulia zaidi kama baba, mtu wa familia, na mfanyabiashara si mhalifu.
Gina anakumbuka changamoto na mafanikio ya uhusiano wao, lakini anasisitiza kuwa kila mara Diddy alipokosea, alikubali makosa yake na alijitahidi kufanya maamuzi bora zaidi baadaye.
Anadai kuwa Diddy alibadilika na kuwa mtu bora na kufikia mwisho wa uhusiano wao, alikuwa amejawa na hali ya upendo, uvumilivu na upole iliyotofautiana sana na tabia yake ya zamani.