Kanye West ashtakiwa, atakiwa kulipa zaidi ya Bilioni 4 kama Fidia

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

9 months ago
rickmedia: kanye-west-ashtakiwa-atakiwa-kulipa-zaidi-bilioni-kama-fidia-357-rickmedia

Kampuni Ya Kupiga Picha Ya ‘Backgrid London Ltd’ Imemfungulia Kesi Rapa Kanye West Kwa Kutumia Picha Zenye Haki Miliki Yao Bila Ridhaa Yao, Na Hivyo Wanadai Fidia Ya Kiasi Cha Zaidi Ya Tsh Bilioni 4+.

Backgrid Wamemshtaki Kanye Kwa Ku-Post Picha 10 Tofauti Zake Pamoja Na Mke Wake Katika Mtandao Wa Instagram Na Tovuti Yake Ya ‘Yeezy’, Wakidai Kwamba Amekiuka Sheria Ya Haki Miliki Lakini Pia Wamepoteza Mamilioni Ya Fedha.

Hivyo Wanadai Fidia Ya Kiasi Cha $150K (Tsh Mil 406/=) Kwa Kila Picha Kati Ya Hizo 10 Ambazo Jumla Inakuwa BILIONI 4, Fedha Ambazo Zitatumika Pia Kuwalipa Wanasheria Wao.