Kinara wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) Raila Odinga amejitokeza kutetea utawala wa Rais William Ruto, na kuutaja kuwa utawala ambao utasaidia kuokoa Wakenya kutokana na matatizo ya kabla ya uhuru.
Akiwahutubia wakaazi wa mji wa Homa Bay Odinga alimiminia serikali sifa kemkem, ambayo alisema sasa inatekeleza kile alichotarajia kufanya kama angekuwa Rais wa Taifa hilo.
"Tulikuwa na haya yote chini ya mpango wetu wa Azimio na sasa tunaona kwamba Wakenya wameiga mfano wetu na hili ni jambo zuri na ninataka raia wetu wamuunge mkono," alisema.