Tamasha la Tatu Mfululizo la Shakira Limepigwa Chini

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

2 days ago
rickmedia: tamasha-tatu-mfululizo-shakira-limepigwa-chini-570-rickmedia

Staa wa Muziki kutoka Colombia #Shakira kwa mara nyingine ameghairisha Tamasha lake, #Shakira alitarajiwa kutumbuiza leo usiku katika Uwanja wa Nationals Park huko Washington D.C., lakini uongozi wa uwanja huo ulitangaza siku ya jana Ijumaa kwamba #Shakira hatapanda jukwaani tena.

#Shakira pia alikuwa na maonyesho mawili huko Boston ambayo yalighairiwa ghafla mapema wiki hii alitarajiwa kutumbuiza katika uwanja wa Fenway Park siku ya Alhamisi na Ijumaa lakini wakaguzi wa jiji walisimamisha maonyesho hayo baada ya ukaguzi wa kawaida wa jukwaa kabla ya onyesho kugundua kuwa baadhi ya vipengele vya muundo wa jukwaa havikukidhi viwango vinavyotakiwa.

Inaonekana matatizo yaliyojitokeza Boston yanasababisha athari hadi Washington D.C., ambako #Shakira alitarajiwa kutumbuiza kama sehemu ya sherehe za makaribisho za #WorldPride, tamasha kubwa zaidi la LGBTQ+ duniani.

Uwanja wa Nationals Park unasema... "Kwa sababu ya matatizo yaliyotokana na onyesho la awali huko Boston, vifaa vyote vya maonyesho ya ziara ya Shakira haviwezi kusafirishwa hadi Washington, D.C. kwa wakati kwa ajili ya tamasha lake lililopangwa kufanyika Jumamosi, Mei 31. Kwa hivyo, onyesho la D.C. limeghairishwa. Licha ya juhudi zote za kulifanya liwezekane, haiwezekani kuendelea kama ilivyopangwa."

Shakira anasema... "Nimekuwa nikihesabu siku, nikiwa na hamu ya kukutana tena na mashabiki wangu wa Washington na Boston, na mimi pamoja na timu yangu tumefanya kila juhudi kuhakikisha linatokea, lakini kwa sasa haitegemei mtu mmoja, na nina uchungu sana kwamba maonyesho haya hayawezekani kwa wakati huu. Naahidi kufanya kila niwezalo kuwa pamoja nanyi haraka iwezekanavyo."

Hakuna taarifa bado iwapo maonyesho ya Boston na D.C. yatapangiwa tarehe nyingine.