Wahamiaji 530,000 Kufukuzwa Marekani

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

2 days ago
rickmedia: wahamiaji-530000-kufukuzwa-marekani-45-rickmedia

Mahakama ya Juu ya Marekani ilitoa uamuzi na kuruhusu Utawala wa Rais Donald Trump kufuta hadhi ya kisheria ya zaidi ya wahamiaji 500,000 wanaoishi Marekani

Uamuzi huo umesimamisha agizo la jaji wa shirikisho la awali la kuzuia utawala kusitisha mpango wa uhamiaji wa ulioanzishwa na Rais wa zamani Joe Biden.

Mpango huo uliwalinda wahamiaji wanaokimbia machafuko ya kiuchumi na kisiasa katika nchi zao.

Agizo hilo jipya linaweka takriban wahamiaji 530,000 kutoka Cuba, Haiti, Nicaragua na Venezuela katika hatari ya kufukuzwa nchini.

Majaji Ketanji Brown Jackson na Sonia Sotomayor, wawili kati ya majaji watatu wa kiliberali wa mahakama hiyo, walipinga.

Utawala wa Trump ulikuwa umewasilisha rufaa ya dharura kwa Mahakama ya Juu baada ya jaji wa shirikisho huko Massachusetts kuzuia utawala kusitisha mpango huo, unaojulikana pia kama msamaha wa kibinadamu wa CHNV.