Kendrick Lamar Amekuwa Rapa Wa Kwanza Kuingiza Mpunga Huu Mrefu kwa Show moja

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

2 days ago
rickmedia: kendrick-lamar-amekuwa-rapa-kwanza-kuingiza-mpunga-huu-mrefu-kwa-show-moja-639-rickmedia

Habari za hivi karibuni zinaonyesha kuwa Rapa #KendrickLamar ameweka rekodi mpya kwa kuwa rapa wa kwanza kupata zaidi ya $14.8M kutoka kwwenye onyesho moja.

Katika tamasha la ufunguzi la ziara yake ya "Grand National Tour" akiwa na #SZA, lililofanyika tarehe 19 Aprili 2025 katika U.S. Bank Stadium, Minneapolis, walikusanya jumla ya $14.8M kutoka kwa watazamaji 47,354, kila tiketi ikiwa na wastani wa bei ya dola 192.70.

Aidha, tamasha hili pia lilikuwa na idadi kubwa ya watazamaji kwa #Kendrick na #SZA, likiwa tamasha lenye uhitaji mkubwa zaidi katika historia yao .