Mradi wa Mji wa Kisasa wa Msanii Aliaune Thiam ‘Akon’ ‘Akon City’, wenye thamani ya Tsh. Trilioni 15.5, umefutwa rasmi baada ya kufeli kukamilisha ujenzi. Serikali ya Senegal imechukua eneo hilo la ardhi na sasa inapanga kuwekeza Tsh. Trilioni 3.1 kujenga Hoteli na Nyumba za Kupanga kwa ajili ya watalii katika eneo hilo lenye utajiri wa fukwe.
Akon City ilipangwa kukamilika Awamu ya Kwanza Mwaka 2023 na Awamu ya Pili Mwaka 2030, lakini ujenzi ulisimama kutokana na janga la UVIKO-19 pamoja na ukosefu wa Fedha. Hadi mwaka 2024, ujenzi ulikuwa umefikia msingi wa jengo la mapokezi pekee.