Mwamamke aliyemshtaki kwa ubakaji rapa JAY-Z amesimama kidete kwa madai yake licha ya kufuta kesi yake. Kama tulivyo ripoti hapo awali, mnamo Februari 14, mwanamke huyo, akijitambulisha kama Jane Doe, na wakili wake, Tony Buzbee, waliondoa kesi yao bila maelezo na ufafanuzi wowote.
Ndani ya saa 48, JAY-Z aliwakashifu Doe na Buzbee, na kisha kuwasilisha rasmi kesi ya kudhalilisha jina lake dhidi ya wakili huyo. Mnamo Februari 25, hakimu alipendekeza kesi hiyo iendelee, akidai ushahidi unaodaiwa unaonyesha Buzbee akishiriki na kuchapisha machapisho ya hatia kwenye mitandao ya kijamii.
Mapema jana (Jumatatu, Machi 3), JAY-Z alifungua rasmi kesi dhidi ya mwanamke huyo aliyefuta kesi ya unyanyasaji wa kingono dhidi yake. Saa kadhaa baadaye, Doe anasimama kidete kwa madai yake licha ya kufuta kesi yake.
Katika hati mpya za kisheria zilizopatikana na TMZ, Doe anasema Jay-Z anajaribu kumdhulumu kwa kusema kwamba madai yake ni ya uzushi. Mwanamke huyo amefichua kuwa aliamua kufuta kesi yake kwa sababu alimwogopa JAY-Z na wafuasi wake; hasa hofu ya kutengwa hadharani na kushambuliwa hadharani.
Mwanamke huyo anadai hivi majuzi alikimbizwa na watu wawili nje ya nyumba yake. Walidai kuwa wachunguzi wanaofanya kazi kwa mmoja wa mawakili wa JAY-Z. Doe anasema walijaribu kumshurutisha kutia sahihi hati ya kiapo inayosema madai yake ya ubakaji dhidi ya Jay-Z ni ya uongo, lakini alikataa.
Pia inadaiwa waliuliza ikiwa Buzbee alimtafuta na kumpa pesa za kusema uwongo kwenye kesi hiyo, Alikanusha madai yote mawili. Makabiliano hayo yanayodaiwa sasa yamemfanya Doe kuogopa na kuingiwa na hofu kutokana na JAY-Z kuona jinsi watu hao walivyogundua utambulisho wake, jambo ambalo halijajulikana katika ripoti za vyombo vya habari na taratibu za kisheria. Doe pia anadai kuwa wazazi wake walifikiwa na wanaodaiwa kuwa wachunguzi wakiuliza maswali sawa kuhusu wakili wake na madai yake.