Mwanasiasa mkongwe, Profesa Philemon Mikol Sarungi amefariki Dunia, leo Machi 5, 2025 ambapo msiba upo nyumbani kwake Oysterbay, Mtaa wa Msasani Jijini Dar es Salaam.
Taarifa ya Familia ya Chifu Sarungi na ukoo wa Nyiratho wa Utegi, Rorya imetangaza msiba huo na kueleza kuwa taarifa na taratibu nyingine zitatolewa na familia.