Baada ya La Liga, UEFA sasa pia imechukua hatua kwa kumsimamisha mwamuzi Munuera Montero kuchezesha mashindano ya Ulaya hadi itakapotangazwa tena.
Montero anatuhumiwa kumtoa nje ya Uwanja Jude Bellingham kwa Kadi nyekundu kimakosa katika mchezo wa La Liga ambao ulitamatika kwa sare ya 1-1 dhidi ya Rayo Vallecano baada ya kupishana lugha Jumamosi Februari 15.