Sera ya Trump ya Wahamiaji, mauzo ya bia yashuka

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 week ago
rickmedia: sera-trump-wahamiaji-mauzo-bia-yashuka-443-rickmedia

Kampuni ya Constellation Brands imeripoti kushuka kwa mauzo ya bia zake maarufu kama Modelo, Corona na Pacifico kwa mara ya kwanza tangu ilipochukua usimamizi wa biashara hiyo mwaka 2013. Kwenye robo ya kwanza ya mwaka huu, mauzo kwa wauzaji wa rejareja yameshuka kwa asilimia 1.

Kwa mujibu wa wachambuzi na wasambazaji wa bia, sababu kuu ya kushuka huko ni hofu inayozidi kuongezeka miongoni mwa wahamiaji wasio na nyaraka, hasa katika maeneo ya California Kusini na Texas. Wahamiaji wengi wanaepuka kununua pombe kwenye maduka ya ulevi kutokana na ulazima wa kuonyesha kitambulisho, jambo linalowaweka kwenye hatari ya kukamatwa na maafisa wa uhamiaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Constellation, Bill Newlands, amesema kuwa baadhi ya wateja wa Latino sasa wanahama kutoka kwenye maduka madogo ya kienyeji na kuelekea kwenye maduka makubwa ya rejareja ili kujichanganya na umati na kuepuka kutiliwa shaka.

Mabadiliko haya ya tabia ya ununuzi yameathiri kwa kiasi kikubwa soko la bia na kuonyesha jinsi siasa za uhamiaji zinavyoweza kuwa na athari pana hata katika biashara za kila siku.