Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Jose Chameleone ametua nchini Tanzania kwa mara ya kwanza baada ya kuugua kwa muda mrefu. Jose ametua nchini Tanzania kwaajili ya shughuli za kimuziki. Baada ya kutua Jose amezungumza na waandishi wa Habari na kufunguka mambo mengi yakiwemo kilichokuwa kinamsumbua mpaka kwenye kutibiwa nchini Marekani.