Mkrugenzi Mtendaji wa TANESCO Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga afariki Dunia kwa ajali

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 week ago
rickmedia: mkrugenzi-mtendaji-tanesco-mhandisi-gissima-nyamo-hanga-afariki-dunia-kwa-ajali-143-rickmedia

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Usambazaji Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Aprili 13, 2025 majira ya Saa 6 hadi Saa 7 usiku katika ajali iliyotokea Wilayani Bunda, Mkoani Mara.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, Pius Lutumo amesema kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya gari la Mkurugenzi lililokuwa likitokea Mwanza kwenda Bunda kugongana uso kwa uso na lori.