Trump akataa Ukraine kushambulia makazi ya Putin

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 day ago
rickmedia: trump-akataa-ukraine-kushambulia-makazi-putin-894-rickmedia

Rais wa Marekani Donald Trump amesema haamini madai kwamba Ukraine ilishambulia makazi ya Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Akizungumza ndani ya Air Force One, alisema kulikuwa na mkanganyiko awali lakini baada ya uchambuzi wa maafisa wa Marekani, walihitimisha kuwa Ukraine haikulenga wala kushambulia makazi hayo.

Marekani imesisitiza umuhimu wa kuthibitisha taarifa kabla ya kutoa hitimisho katika mzozo unaoendelea kati ya Urusi na Ukraine.