Serikali ya mpito ya Venezuela yaomba mazungumzo na Marekani

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 day ago
rickmedia: serikali-mpito-venezuela-yaomba-mazungumzo-marekani-168-rickmedia

Serikali ya mpito ya Venezuela, kupitia Rais Delcy Rodríguez, imetoa ujumbe kwa jumuiya ya kimataifa na Marekani ikisisitiza dhamira ya kudumisha amani, kuheshimiana na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa bila vitisho, siku moja baada ya kukamatwa kwa Rais Nicolas Maduro na vikosi vya Marekani.

Rodríguez amesema Venezuela inaamini amani ya dunia huanzia na amani ya ndani, na imeitaka Marekani kuingia katika mazungumzo ya amani kwa ajili ya ajenda ya maendeleo ya pamoja chini ya sheria za kimataifa.