Msanii Shilole apata ajali ya gari baada ya gari lake kugongana na ng'ombe

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

11 hours ago
rickmedia: msanii-shilole-apata-ajali-gari-baada-gari-lake-kugongana-ngombe-272-rickmedia

Msanii na Mjasiriamali Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amepata ajali mbaya ya gari jana usiku alipokuwa akitokea Mkoani Kigoma kurudi Dodoma, taarifa hiyo imetolewa na Mbunge wa Kigoma Mjini Mheshimiwa  Clayton Revocatus Chipando maarufu kama Baba Levo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Baba Levo ameweka wazi kuwa ajali hiyo imesababishwa na gari la Shilole aina ya Alphad kugongana na Ng'ombe maeneo ya Malagarasi Mkoani Kigoma, mpaka sasa Shilole yuko hospital Mkoani Tabora akipatiwa matibabu na wanaendelea kufuatilia maendeleo yake ya kiafya kwa ukaribu sana.

Shilole alikuwa akitokea Mkoani Kigoma kwenye jambo la Mbunge wa Kigoma Mjini Baba Levo "Pilau Day" ambapo alikuwa akipika pilau kwaajili ya wananchi wa Kigoma walipowekewa chakula na Mbunge wao kwaajili ya kusheherekea Mwaka mpya pamoja.

Get Well Soon Shilole