Rais wa Gabon aanza mwaka 2026 kwa mabadiliko ya viongozi Serikalini

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

16 hours ago
rickmedia: rais-gabon-aanza-mwaka-2026-kwa-mabadiliko-viongozi-serikalini-523-rickmedia

Rais wa Gabon, Brice Nguema, ameaanza Mwaka Mpya wa 2026 kwa kufanya mabadiliko ya uongozi serikalini.

Mtandao wa African News umeeleza kwamba, hatua hiyo ni mkakati wake katika kujiimarisha kisiasa tangu Nguema aliposhika madaraka mwaka 2023.

Jana Januari 2, 2026 Rais Nguema amemteua Hughes Chambrier kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri, huku Hermann Immongault akitolewa Wizara ya Mambo ya Ndani na kuteuliwa kuw Makamu wa Rais wa Serikali.

Kupandishwa cheo kwa Immongaultni kutokana umahiri wake namna alivyosimamia uchaguzi wa wabunge na maseneta uliofanyika Septemba 2025, uliokipa chama cha Nguema cha Democratic Union of Builders kushinda viti 101 kati ya viti 145 vya Bunge.

Nguema pia amesaini amri rasmi inayothibitisha muundo wa serikali mpya. Serikali yake sasa ina mawaziri 31, kutoka 30 awali, ambapo mawaziri 10 ni wanawake.

Nguema alishinda uchaguzi wa urais mwezi Aprili mwaka jana, ikiwa ni miaka miwili baada ya kuongoza mapinduzi ya kijeshi yaliyomaliza miaka 55 ya utawala wa familia ya Bongo nchini humo.