Will Smith na kampuni yake washtakiwa kwa unyanyasaji wa kijinsia

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

16 hours ago
rickmedia: will-smith-kampuni-yake-washtakiwa-kwa-unyanyasaji-kijinsia-513-rickmedia

Muigizaji wa Marekani Will Smith na kampuni yake ya Treyball Studios Management Inc wamefunguliwa mashtaka ya madai ya unyanyasaji wa kingono na mpiga violin Brian King Joseph.

Brian anadai alialikwa kushiriki ziara ya dunia ya “Based on a True Story: 2025” na kudai kulikuwa na vitendo vya kumwandaa kwa lengo la kumtumia kingono baadaye.

Pia anasema kuwa Machi 2025 alikuta chumba chake cha hoteli kimeingiliwa bila ruhusa na kuacha vitu na ujumbe wa kutisha, hali iliyomletea hofu na msongo wa mawazo. Kesi hiyo iko katika Mahakama ya Los Angeles, huku madai hayo yakisubiri kusikilizwa.