Msanii wa Hip-Hop ambaye pia ni Naibu Waziri Wa Utamaduni Sanaa na Michezo nchini Mheshimiwa Hamis Mwinjuma au kama kwenye sanaa anavyofahamika kwa jina la Mwana FA ameachia orodha ya nyimbo alizosikiliza zaidi mwaka uliopita 2025 huku orodha hiyo ikijaa wasanii wa kizazi kipya na ikiwa na uhaba wa nyimbo za Hip-Hop.
Mwana FA kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka orodha hiyo huku wasanii kama Mbosso,Marioo,Maua Sama,Frida Amani,Pateni, na wengine wakionekana kwenye orodha hiyo na Mbosso na wimbo wake wa Pawa ndiye aliyeifungua orodha hiyo huku Harmonize akiifunga na wimbo wake wa Furaha.
Kwenye post hiyo watu mbalimbali wameacha maoni yao huku wengi wakisema wasanii wa Hip-Hop wanapaswa kujitafakari kwasababu kwenye orodha ya mwana Hip-Hop mwenzao ila nyimbo zao zimekuwa haba ina maana wamekuwa na uhaba wa kufanya kazi.
Msanii kama Lulu Diva ameacha maoni yake kwa kuandika "Nimelia sanaaaaa yangu haipoooo😢😢😂😂😂😂" japo Mwana FA hajajibu lolote huku Mbosso akiacha maoni yake kwa kuandika "Kaka Mkubwa 🙏" na Mwana FA kumjibu "@mbosso_ wewe na chenji imebaki Mbosso mdogo wangu,noma sana 👏"
Je wewe orodha ya nyimbo ulizozisikiliza 2025 ni ipi?