Klabu ya Manchester United imemfuta kazi kocha wake raia wa Ureno, Ruben Amorim, kutokana na muendelezo wa matokeo yasiyoridhisha akimalizia kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Leeds United jana Jumapili.
Mchezo huo umekuwa wa mwisho kwa Amorim ndani ya kipindi chake cha miezi 14 akiwa Old Trafford tangu alipojiunga nao Novemba 2024.
Kocha huyo ameondoka kufuatia mvutano uliokuwepo kati yake na uongozi wa klabu.
Aliyekuwa kiungo wa zamani wa United na kwa sasa kocha wa kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 18, Darren Fletcher, anatarajiwa kupewa mikoba ya ukocha kwa muda.
Kwa mujibu wa mkataba alioingia na United Novemba 2024, hakuna kipengele cha klabu kumlipa fidia iliyopunguzwa. Hivyo, United italazimika kulipa mshahara wake wote hadi mwisho wa mkataba wake uliokuwa unatarajiwa kuisha mwaka 2027, ukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.