Watu wengi waliamini kuwa Mwigizaji Jackline Wolper na mume wake Rich Mitindo walimaliza tofauti zao na kuendelea kuishi pamoja kama familia, japo wengi tunafahamu kuwa Rich mitindo huwa anaishi China na Tanzania huwa anakuja mara chache tu na Wolper ameridhia hilo,kumbe mambo yako tofauti.
Kupitia podcast ya A-List ambayo inawajumuisha Jackline Wolper,Irene Uwoya,Kajala Masanja na Aunt Ezekiel, Wolper ameelezea machungu yake namna ambavyo alikuwa tayari kushirikiana na mumewe kwenye mambo ya maendeleo lakini mumewe amekuwa akirudisha nyuma maendeleo yao.
Kwanza ameonyesha kusikitishwa na kitendo cha mume wake muda mwingi kuishi nchini China kuliko Tanzania na akirudi anarudi bila pesa, Wolper anasema Rich Mitindo huwa anakaa China Miezi 7 na kurudi Tanzania kwa miezi 3 tu.
Muda ambao Rich anakaa China ni muda ambao hata yeye pia huwa anahitaji kuwa na mwanaume ambaye anamsaidia usimamizi wa biashara zake na ndio sababu ya kusema kwenye kipindi kuwa angepewa nafasi ya kuweka vitu kwenye kapu moja basi ombi lake lingekuwa apate mwanaume (Rafiki wa Kiume).
Kwa upande mwingine Wolper anasema uzembe wa Rich kwenye biashara ulisababisha wao kufunga biashara yao ya mat-shirts pamoja na biashara yao ya suti.
Tazama Hapa Chini👇🏾