Taarifa ya msanii Shilole kupata ajali ilitolewa na Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Clayton Revocatus Chipando maarufu kama Babalevo ambaye alimpa Shilole tenda ya kupika siku ya Mwaka Mpya jimboni kwake kwenye siku aliyoipa jina la "Pilau Day" na kwenye taarifa yake Babalevo aliweka wazi kuwa Shilole alipata ajali akiwa anatokea Mkoani Kigoma kuelekea Dodoma.
Kwenye post hii ya Shilole amemshukuru Mungu kwa kumvusha salama kwenye ajali hiyo huku akikiri wazi kuwa kupitia changamoto hii ameiona neema ya Mungu kwa macho yake. Amewashukuru watu wote kwa maombi yao huku akisisitiza Mungu ni mwema sana.
Shilole alipata ajali eneo la Maragalasi Mkoani kigoma baada ya gari lake aina ya Alphad kugongana na ng'ombe, hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Babalevo.