Rapa Boosie BadAzz akabiliwa na kifungo cha Miaka 2 Jela

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 day ago
rickmedia: rapa-boosie-badazz-akabiliwa-kifungo-cha-miaka-jela-518-rickmedia

Rapa Wa Marekani ‘Boosie BadAzz’ anatarajiwa kuhukumiwa wiki hii katika kesi yake Ya kumiliki silaha kinyume Cha Sheria.

Waendesha mashtaka wanapendekeza ahukumiwe kifungo cha miaka 2 (miezi 24) gerezani. Lakini Pia Baada ya kutoka gerezani, wanataka awe chini ya uangalizi wa serikali kwa miaka 3 (supervised release). Hukumu Yake Itasoma Januari 9.

Kama Unakumbuka Mwaka 2023, Boosie alikamatwa Huko San Diego baada ya polisi kuona bunduki kwenye kiuno chake Wakati Akiwa Instagram Live. Baadaye polisi Walifika Eneo La Tukio Na Kulikagua gari lake na Kumkuta Akiwa Na silaha kadhaa.

Agosti 2025, Rapa Huyu alikubali makubaliano ya kosa (plea deal) katika kesi hiyo Ili apunguziwe Adhabu. Kwa sasa Boosie anatumaini kupata msamaha (pardon) kutoka kwa Rais Donald Trump, jambo ambalo lingeweza kumsaidia kuepuka au kupunguza adhabu Yake.