Serikali ya Cuba imesema raia 32 wa Cuba wamefariki dunia kufuatia mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na vikosi vya Marekani nchini Venezuela mapema Jumamosi.
Katika operesheni hiyo, Rais wa Venezuela Nicolás Maduro na mkewe Cilia Flores walikamatwa. Rais wa Cuba Miguel Díaz-Canel ametangaza siku mbili za maombolezo. Awali, Waziri wa Ulinzi wa Venezuela aliripoti kuwa walinzi kadhaa wa Maduro waliuawa wakati wa operesheni hiyo.
Maduro anatarajiwa kufikishwa mahakamani nchini Marekani leo.