Ole Gunnar Solskjær mbioni kuirudia Klabu yake ya zamani, Manchester United

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 day ago
rickmedia: ole-gunnar-solskjaer-mbioni-kuirudia-klabu-yake-zamani-manchester-united-66-rickmedia

Ole Gunnar Solskjær ameonyesha nia ya kurejea Manchester United kama kocha wa mpito (caretaker manager) hadi mwisho wa msimu.

Uongozi wa Manchester United umejulishwa kuwa Ole yuko tayari kurejea, bila kujali muda wa mkataba.

Manchester United wanachukua muda wao kutathmini makocha wengineambao CV zao zimefikishwa mezani kwa nafasi ya muda mfupi katika saa au siku zijazo.

Iwapo hilo litatokea, United wataendelea kumsaka na kumteua kocha wa kudumu msimu wa kiangazi kwa ajili ya msimu wa 2026/27.

Kwa sasa, Darren Fletcher ndiye kocha wa muda wiki hii.