Mohamed Salah amesaini Mkataba wa Miaka 2 kuendelea kubaki Liverpool

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 week ago
rickmedia: mohamed-salah-amesaini-mkataba-miaka-kuendelea-kubaki-liverpool-791-rickmedia

Hatimaye Mshambuliaji, Mohamed Salah amesaini mkataba mpya kuendelea kubaki Liverpool kwa mshahara wa Pauni 350,000 (Tsh. Bilioni 1.2) kwa wiki baada ya mvutano wa muda mrefu kuhusu suala la Mkataba wake ambao ulitarajiwa kumalizika Juni 2025.

Baada ya kusaini amesema “Nimefurahi, tuna timu nzuri, tuna nafasi ya kushinda mataji mengine, nimecheza hapa kwa Miaka Nane, naamini nitatimiza Miaka 10.”

Salah (31) amefunga Magoli 243 katika mechi 394 alizoichezea Liverpool, msimu huu katika Premier League amefunga Magoli 27 na Asisti 17.

Taarifa hii kutoka Klabu ya Liverpool imekuja kuzima minong'ono ya miezi kadhaa kuwa Mo Salah anaondoka kwenye klabu hiyo kwenda Uarabuni, hii ni habari njema kwa mashabiki wa Liverpool na mashabiki wa Mo Salah mwenyewe, Chuma bado kipo Liverpool kwa miaka 2.