Bilioni 83 za Marehemu Liam Zitasimamiwa na Mzazi Mwenzie Ambae Waliachana Kabla ya Umauti.

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

6 hours ago
rickmedia: bilioni-marehemu-liam-zitasimamiwa-mzazi-mwenzie-ambae-waliachana-kabla-umauti-994-rickmedia

 Imewekwa wazi kuwa Marehemu #Liam ambae zamani alikuwa mmoja ya Wasanii wanaounda Kundi la #OneDirection aliacha Kiasi cha Pesa cha €28.2 M (TSH. Bilioni 83) kwa Mtoto wake (Bear) Na saaa Ni Rasmi zitasimamiwa Na Mzazi mwenzie #Cheryl ambae walikuwa wameshaachana.

Mwimbaji huyo aliyekuwa na umri wa miaka 31 alifariki dunia baada ya kudondoka kutoka kwenye balkoni ya hoteli nchini Argentina kufuatia msururu wa matumizi ya pombe na dawa za kulevya mwezi Oktoba.

#Bear, akiwa mtoto wa damu wa Liam, atapokea urithi wake wa £28.5 milioni, ambao ulipunguzwa hadi £24.2 milioni baada ya kulipwa kwa gharama na madeni. Hati za mahakama zinaonyesha kuwa #Payne alimpa #Cheryl, mwenye umri wa miaka 41, mamlaka ya kusimamia urithi wake, licha ya kwamba walitengana kabla Bear hajafikisha miaka miwili.

#Cheryl alitajwa pamoja na Richard Bray, wakili maarufu wa muziki ambaye amewahi kuwatetea wasanii wakubwa wakiwemo Ed Sheeran.