EX wa Rapa #Diddy, #CassieVentura ambae kwa sasa ni Mjamzito Aonekana Siku 4 Kabla ya Kesi ya Biashara ya Ngono ya #Diddy Kuanza New York.
#Ventura ni miongoni Mwa wanaotarajiwa kutoa ushahidi mahakamani akitumia jina lake halisi.
Mwanasheria wa Ventura, Douglas H. Wigdor, aliambia jarida la PEOPLE mwaka 2024 kuhusu shambulio la Diddy dhidi ya mteja wake.
Cassie Ventura, shahidi mkuu wa serikali katika kesi ya shirikisho dhidi ya mpenzi wake wa zamani Sean "Diddy" Combs, alionekana jijini New York akiwa mjamzito na mtoto wake wa tatu siku ya Jumatano, Mei 7. Kesi ya Diddy inatarajiwa kuanza kwa hotuba za ufunguzi Mei 12.
Ventura ameolewa na Alex Fine kwa miaka sita na sasa anatarajia mtoto wao wa tatu. Alianza kuonesha uhusiano wao kwa mara ya kwanza Desemba 2018, miezi miwili baada ya kuthibitisha kuvunjika kwa uhusiano wake na Diddy. Wawili hao walifunga ndoa mwezi Agosti uliofuata na wakampokea binti yao wa kwanza, Frankie, Desemba 2019 na binti wao wa pili, Sunny, Machi 2021.