Klabu ya Simba kutoka nchini Tanzania imefanikiwa kutinga hatua ya Fainali ya kombe la Shirikisho Barani Afrika baada ya kutoka sare na klabu ya Stellen Bosch ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa marudiano ya nusu fainali.
Simba imetinga Fainali kutokana na ushindi wa bao Moja ililolipata kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali, mchezo uliochezwa visiwani Zanzibar.
Kwa maana hii Simba inaweza kucheza Fainali na RSB Berkane au CS Constantine ambao mchezo wao unatarajiwa kupigwa usiku wa April 27,2025.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mechi kocha wa Simba Fadlu Davids amesema kuwa "Sitaki tusherehekee kwa kufika fainali, wacha tujaribu kushinda taji kisha ndio tufurahi"