Prof. Anna Tibaijuka aipa Onyo Tanzania mgogoro na Malawi

-rickmedia: Rick

Rick

20 hours ago
rickmedia: prof-anna-tibaijuka-aipa-onyo-tanzania-mgogoro-malawi-437-rickmedia

Waziri wa Zamani wa Ardhi Prof. Anna Tibaijuka ameipa tahadhari Tanzania juu ya uamuzi wa kuizuia nchi ya Malawi kupitisha bidhaa zake Bandari ya Dar es Salaam baada ya Malawi kutangaza kuzuia bidhaa za Kilimo kutoka Tanzania. Tibaijuka anadai kuwa licha ya Tanzania kuchokozwa kwenye sakata hilo lakini sheria za Kimataifa zinaweza kuja kuidhibu Tanzania kwa kuitoza faini.

Tibaijuka ameandika haya kupitia ukurasa wake wa X zamani Twitter "“Hairuhusiwi ubaguzi wowote unaopendelea bidhaa za nchi inayotoa njia ya kupita au nchi nyingine, hakuna ushuru au kodi ya forodha inayopaswa kutozwa bidhaa zilizoko njiani isipokuwa kwa gharama halali za kiutawala, maana Tanzania hairuhusiwi kisheria kuzuia au kuchelewesha bidhaa za Malawi kama njia ya kulipiza kisasi, ikiwa Tanzania ilikuwa na malalamiko, ilikuwa lazima ipitie utaratibu wa WTO, au SADC si hatua za upande mmoja, pili Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Sheria ya Bahari (UNCLOS), Sehemu ya X (Ibara 124–132) inalinda haki za nchi zisizo na bandari kwa nguvu”

“Pia Ibara ya 125, nchi zisizo na bandari zina haki ya kupitisha bidhaa zao kwa uhuru kupitia nchi jirani kwa kutumia aina yoyote ya usafiri, nchi jirani hazipaswi kuweka vizuizi visivyohitajika wala kudhoofisha usafirishaji huo, Malawi na Tanzania zote ni wanachama wa UNCLOS, hivyo haki hii ina nguvu ya kisheria ya kimataifa.“Kabla ya kuhamia Nairobi kama Mkurugenzi wa UNHABITAT nilikuwa Mkurugenzi Mratibu wa maswala haya huko UNCTAD/WTO Geneva”

Kauli ya Tibaijuka inakuja siku moja tangi Serikali ya Tanzania kupitia Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, itoe tamko la kupiga marufuku mazao ya kilimo kutoka Nchi za Afrika Kusini na Malawi baada ya Nchi hizo mbili kuzuia mazao kutoka Tanzania.