Ally Kamwe akamatwa kwa tuhuma za kutoa kauli chafu kwa viongozi wa Serikali

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 day ago
rickmedia: ally-kamwe-akamatwa-kwa-tuhuma-kutoa-kauli-chafu-kwa-viongozi-serikali-874-rickmedia

Afisa Habari wa Timu ya Yanga SC, Ali Kamwe, amekamatwa na kuwekwa Mahabusu kutokana na tuhuma za kutoa kauli zisizo nzuri kwa Viongozi wa Serikali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, RPC Richard Abwao, amethibitisha kwa kusema "Nathibitisha tunamshikilia msemaji wa Yanga Ali kamwe, tunamshutumu kwa kutoa kauli mbaya dhidi ya Viongozi wa Serikali, tunaendelea na mahojiano nae na tutatoa taarifa”.

Ikumbukwe Timu ya Yanga ilikuwa Mkoani Tabora Aprili 2, 2025 kwa ajili ya Mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa dhidi ya Tabora United ambapo Yanga walishinda 3-0, ambapo kabla ya Mchezo, Ali alitoa kauli kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, ambaye aliahidi Tsh. milioni 60 kwa Tabora wakiifunga Yanga.