Afisa habari wa Timu ya Mpira Yanga Ali Kamwe aachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa na jeshi la polisi mkoani Tabora kwa tuhuma za kutoa lugha chafu kwa viongozi kama ilivyothibitishwa na RPC Richard Abwao baada ya kumuita kwa mahojiano maalumu.
Inaelezwa kuwa Ali Kamwe amepewa onyo na kufikia makubaliano na jeshi la polisi na sasa yupo huru kwa dhamana ila anatakiwa kuripoti April 21,2025.