AC Wazalendo: Vitendo vya ukatili vya Mamlaka ya Hifadhi dhidi ya wananchi vimezidi

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

6 days ago
rickmedia: wazalendo-vitendo-vya-ukatili-vya-mamlaka-hifadhi-dhidi-wananchi-vimezidi-472-rickmedia

Naibu Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii ACT Wazalendo, Anthony Ishika amesema matukio ya uvunjifu wa Haki za Binadamu yanayofanywa na Mamlaka za Hifadhi yameongezeka ikiwemo kuuawa kwa risasi za moto mfano ilivyotokea kwa John James (35) wa Chanika (Dar), kuchomwa na kubomolewa nyumba za Wakazi wa Bondo, Kilindi (Tanga), kuvamiwa na kuvunjwa kwa Makazi ya Watu Mlimba (Morogoro).

Amesema “ACT inalaani vikali mwendelezo wa ukatili na unyanyasaji wa Wananchi unaofanywa na Mamlaka za Hifadhi Nchini ambazo ni Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Mamlaka ya Wanyama Pori (TAWA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa (TANAPA) huku Waziri wa Maliasili na Utalii, Pindi Chana akishindwa kuchukua hatua stahiki.”

Ameongeza kuwa ACT inamtaka Waziri Pindi Chana ajiuzulu kwa kushindwa kuzuia vitendo wanavyofanyiwa Wananchi, uchunguzi huru ufanyike, operesheni zote za dhuluma zinazoendelea dhidi ya Wananchi kwenye maeneo yao ya asili na fidia itolewe kwa waathirika wa ukatili na wahakikishiwe vitendo hivyo havitarudiwa.