Taarifa ya Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Young Africans SC, Andre Mtine, imesema Mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Simba (Derby) ya leo saa 1 usiku ipo palepale na Uongozi utapeleka timu uwanja wa Benjamin Mkapa kama inavyoelekezwa kwenye kanuni, na pia hawatakuwa tayari kucheza mchezo huo siku nyingine tofauti na leo.
Hatua hiyo ni baada ya klabu ya Simba SC kutangaza kuwa haitocheza mchezo wa leo dhidi ya Yanga, kutokana na kuzuiwa kufanya mazoezi katika uwanja wa Benjamin Mkapa usiku Machi 7, 2025.
Taarifa hiyo imeeleza zaidi kuwa Yanga kama wenyeji wa mchezo, wanaamini taratibu zote za mchezo ziko sawa na maandalizi yote yako tayari, hivyi kuwaalika Uwanjani Wanachama, Mashabiki, Wapenzi wa Klabu hiyo kushuhudia mechi hiyo.