Israel inajiandaa kupokea miili ya mateka wanne waliofariki kutoka Gaza siku ya Alhamisi kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano na Hamas Kwamujibu wa vyombo vya Habari vya Nchini humo
Vyombo vya Habari vya Nchini humo vinaeleza kuwa vikosi vya Jeshi la Israeli vimeanza maandalizi ya kupokea miili ya mateka, ambao majina yao bado hayajawekwa wazi.
Kundi la upinzani la Palestina Hamas linatarajiwa kutangaza majina ya wafungwa waliofariki Alhamisi asubuhi, huku miili yao ikipangwa kurejeshwa baadaye siku hiyo hiyo.
Magari ya kubebea wagonjwa ya jeshi la Israel yatasubiri katika kituo maalumu cha mkutano ili kuopoa miili hiyo, ambayo itasafirishwa hadi katika taasisi ya uchunguzi wa kitaalamu nchini humo kwa ajili ya kutambuliwa ambapo mamlaka itatoa taarifa ya mwisho kwa familia za wafungwa.