Kusitishwa kwa msaada huo kutaendelea hadi Trump atakapojiridhisha kuwa Zelenskyy amejitolea kuanzisha mazungumzo ya amani, hatua ambayo inamlazimisha kwenda kwenye meza ya mazungumzo kwa hofu ya kupoteza msaada zaidi wa kijeshi.
Imeelezwa katika wiki za hivi karibuni, Trump ameonesha msimamo unaofanana na Rais wa Urusi, Vladimir Putin kwa madai ya kuwa Ukraine ilianzisha vita na kumshutumu Zelenskyy kuwa Dikteta, hivyo uamuzi wake wa kusimamisha msaada wa kijeshi unaweza kuwa na athari kubwa kwenye mwelekeo wa vita na kumpa Putin nguvu zaidi.