NACADA Yaongeza Muda wa Uhalali wa Kutumia Pombe hadi Miaka 21

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

7 months ago
rickmedia: nacada-yaongeza-muda-uhalali-kutumia-pombe-hadi-miaka-607-rickmedia

Mamlaka ya Kitaifa ya Kukabiliana na Matumizi ya Dawa za Kulevya (NACADA) nchini Kenya imeongeza rasmi umri halali wa ununuzi, uuzaji na unywaji wa pombe kutoka miaka 18 hadi miaka 21. 

Hatua hii inalenga kupunguza upatikanaji wa vileo kwa vijana na kukabiliana na ongezeko la matumizi ya dawa za kulevya na pombe miongoni mwao.

Kupitia tamko rasmi lililotolewa leo, NACADA imeeleza kuwa mabadiliko haya ni sehemu ya mkakati mpana wa kulinda afya ya vijana na kudhibiti athari za kijamii na kiafya zitokanazo na matumizi ya vileo mapema. 

Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha ongezeko la kesi za uraibu na madhara ya kiafya kwa vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 20.