Msanii wa nyimbo za injili #AlexApoko, anayefahamika kwa jina maarufu la #Ringtone, ameachiliwa kwa dhamana ya Tsh.Milioni 56 (Ksh.Milioni 3) au kwa njia mbadala ya dhamana ya pesa taslimu ya Ksh. milioni 1 katika kesi inayomkabili ya madai ya kumtapeli mfanyabiashara mwanamke kipande cha ardhi chenye thamani ya Ksh. milioni 50 katika eneo la Karen, jijini Nairobi Nchini Kenya.
#Ringtone alitumia mwisho wa wiki kizuizini baada ya kufikishwa mahakamani Alhamisi, kufuatia kutolewa kwa hati ya kumkamata kwa kushindwa kuhudhuria vikao kadhaa vya mahakama.
Hii ilikuwa baada ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa Mahakama ya Milimani, #DolphinaAlego, kukataa kuwaachilia #Apoko na mshatakiwa mwenzake, #AlfredJumaAyora, kwa dhamana, baada ya wao kujitetea kuwa hawakuwa na hatia katika mashtaka ya kula njama ya kumtapeli mfanyabiashara #TeresiaAdhiamboOdhiambo.
Kifungu cha mashtaka kilionyesha kuwa walikula njama tarehe au kabla ya Februari 28, 2023, kumtapeli Teresia ardhi yenye ukubwa wa hekta 0.1908 (sawa na ekari 0.47).
Inadaiwa kuwa #Ringtone alitaka kumiliki ardhi hiyo kupitia madai ya umiliki wa muda mrefu (adverse possession), akidai kwamba ameishi kwenye kipande hicho cha ardhi kilichoko Karen kwa zaidi ya miaka ishirini.
#Ayora, ambaye alisomewa mashtaka tarehe 28 Machi, anakabiliwa na shtaka la pili la kutoa taarifa za uongo.