Loading...

Shilole na Mume Wake Ndio Basi Tena, Rommy Athibitisha Ndoa Kuvunjika.

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

3 weeks ago
rickmedia: shilole-mume-wake-ndio-basi-tena-rommy-athibitisha-ndoa-kuvunjika-241-rickmedia

Baada ya kuvuma Stori kwenye Mitandao ya kijamii kuwa kwa Sasa Msanii na Mfanyabiashara Zena Yusuf Mohammed (Shilole) Yupo kwenye penzi jipya na kuwa yeye na Mume wake kwa sasa hawapiki chungu kimoja, Imethibitishwa kuwa ni kweli.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Mpiga picha na Mume wa Shilole, Rommy 3D amelithibitisha hilo huku akisema kuwa amekubali kumpisha kijana mwenzie kwenye kiti hicho na yeye amefua kofia.

Rommy ameandika.. "Habari.....Ndugu zangu kama ambavyo mmeona kwenye mitandao na hiyo ndio hali halisi basi Mimi na aliyekuwa mwenzangu Zuwena Mohamed(Shilole)Naona tumefikia Mwisho na si Vibaya nikakubali matokeo na kumpisha Kijana mwenzangu aendeleze gurudumu hili, na Maisha yaendelee... nipende kutoa shukrani zangu za dhati kwa vile tulivyoishi siku zote za mapenzi yetu 🙏🏽,

Wabillah Tawfiq"