Watengeneza maudhi ya TikTok wa Rwanda kuanza kulipwa kutokana na watu wanavyotazama video zao. Hatua hii imekuja baada ya Rais wa Rwanda Paul Kagame kuweka mkazo kwa mtandao huo kuanza kuwalipa watengeneza maudhui kupitia mtandao huo.
Siku ya February 6 ambapo ilikuwa siku ya Baraza la Kitaifa la Umushyikirano Vijana walimuomba Rais Kagame kuingiliana kati ili mitandao ya kijamii ianze kulipa watengeneza maudhui wa nchini humo.
Akiwa mmoja wa vijana waliopewa nafasi ya kuzungumza mbele ya Rais Kagame Mwanamuziki Bruce Melodie aliweka wazi changamoto hiyo ya watengeneza maudhui kutolipwa na mitandao hiyo.
Taarifa kutoka TikTok ni kwamba kwa sasa watengeneza maudhui kutoka wameanza kuingiza pesa kupitia maudhui hayo .