Mwijaku, mtangazaji na mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, amemwandikia Zaiylisa ujumbe mzito unaogusa hisia na kutia moyo, katika kipindi ambacho mrembo huyo yuko katikati ya sakata na aliyekuwa mume wake, Haji Manara.
Kupitia maneno yenye tafakari ya maisha, Mwijaku alimwambia Zaiylisa:
“Unapofanikiwa kuondoka kwa mtu ambaye hakuwa kwa ajili yako, MUNGU huanza kukubariki kwa mambo ambayo alikuwa akitaka kukufanyia. Hata siku moja usijute kwa yale yaliyotokea kipindi cha nyuma…”
Akaongeza kuwa huzuni na maumivu yaliyopita yalikuwa na sababu njema kimaisha, na kwamba muda wa Mungu ndio bora zaidi:
“Mambo ambayo yalikuletea huzuni na kuugua moyo, yalitokea kwa makusudi iliyo njema kabisa. Siku zote tulia, jitafute, na kaa tayari kupokea baraka za Mwenyezi Mungu. "MUDA WA MUNGU NI BORA."
Katika kipindi ambacho mitandao imejaa drama na kejeli, ujumbe huu unatafsiriwa kama chemchemi ya utulivu, upendo, na matumaini kwa Zaiylisa.