Muziki ni lugha nyepesi zaidi ya watu kuwasiliana na kuelewana vizuri kabisa, huenda hii ndio sababu ya mastaa wakubwa wa muziki kutoka Nigeria Wizkid na Asake kupanga kuchia Extended Playlist 'EP' ya pamoja walioipa jina la 'REAL' ikiwa na jumla ya nyimbo 4 na tayari wimbo mmoja 'Jogodo' wameuachia rasmi kutoka kwenye EP hiyo.
EP ya 'REAL' inatarajiwa kuachiwa January 23, 2026 na itabeba nyimbo nne ambazo ni 1. Turbulence 2. Jogodo 3. Iskolodo 4. Alaye , wimbo wa pili 'Jogodo' tayari umeachiwa watu wanaendelea kuburudika nao.
Hii si mara ya kwanza kwa Wizkid na Asake kushirikiana kwenye wimbo, wawili hao walikutana kwenye wimbo wa Asake 'MMS' mwezi Oktoba mwaka 2024 na mwezi Novemba mwaka huo huo Wizkid akamshirikisha Asake kwenye wimbo wake wa 'Bad Girl'.
Isikilize 'Jogodo' hapa chini 👇🏾