Boss wa Telegram atoka Rumande huko Ufaransa

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

8 months ago
rickmedia: boss-telegram-atoka-rumande-huko-ufaransa-787-rickmedia

Bosi na mwanzilishi wa Telegram Pavel Durov amewekwa chini ya uchunguzi maalumu baada ya kuachiwa kutoka rumande alikokaa kwa siku nne.

Pavel yupo nje kwa dhamana ya Dola Milioni 5.6 ambazo ni sawa na Zaidi ya Bilioni 12 za Kitanzania. Bilionea huyo ambaye ni mzaliwa wa Urusi na Raia wa UFARANSA atatakiwa kuripoti kituo cha Polisi mara mbili kwa wiki na hatoruhusiwa kuondoka kwenye ardhi ya Ufaransa.

Pavel alikamatwa siku nne zilizopita baada ya kutua uwanja wa ndege wa Le Bourget nchini Ufaransa na kufunguliwa mashtaka ya Uhalifu yanayofanyika kupitia mtandao wake wa Telegram kama Utakatishaji Pesa, magenge ya kihalifu n.k.