Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Jumanne Muliro, ametoa wito kwa Watanzania kutokushabikia vurugu akisisitiza kuwa zina gharama kubwa.
Akizungumza kwenye mkutano wa RC Chalamila na Wahariri, amesema Polisi inatambua wajibu wake wa kulinda amani na kuhakikisha wananchi wanafanya shughuli zao bila hofu.
Muliro amewataka wanahabari kutekeleza majukumu yao kwa usalama, akiahidi kuwa Polisi itaboresha upatikanaji wa taarifa ili kuepusha taharuki.
Aidha, amesisitiza kuwa nchi ni ya wote, hivyo kila mtu anapaswa kuheshimu sheria na kuepuka vitendo vinavyoweza kuleta vurugu.