Watu wawili wa Kitongoji cha Itwili, Kijiji cha Old Shinyanga, Mama Suzana Samweli (41) na binti yake Happyness Peter (20) wamefariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi walipokuwa wakichimba kokoto katika eneo lisilo rasmi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi, amethibitisha tukio hilo na kusema miili imehifadhiwa Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa kijiji, Bw. Doto Bwire, ameonya wananchi dhidi ya uchimbaji kwenye maeneo hatarishi na yasiyoruhusiwa kisheria.